Prime Minister At WCFMfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi utazindua huduma za utoaji mafao ya fidia tarehe 20 Desemba 2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Kisenga LAPF, uliopo jengo jipya la LAPF, Kijitonyama, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).

Mafao yanayotolewa na Mfuko ni pamoja na; huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha, msaada wa mazishi na malipo kwa wategemezi.

Rehema Lecturing At WCF Seminar

Uzinduzi huu ni wa kihistoria nchini ambapo tunashuhudia kupanuka kwa huduma za hifadhi ya jamii na Mfuko kuanza rasmi ulipaji mafao kwa wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na sekta Binafsi ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa “FIDIA STAHIKI, KWA WAKATI NA  KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU”