Namna ya kufanya miamala
Waajiri wote katika Sekta rasmi ya Umma na Binafsi Tanzania Bara wanatakiwa kuchangia katika Mfuko ambapo michango katika sekta binafsi ni asilimia 0.5% na sekta ya umma asilimia 0.5% ya mapato ya mfanyakazi kila mwezi. Mambo muhimu ya kuzingatia katika uchangiaji ni:
a)Mwajiri anaweza kulipa katika Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) baada ya kupata kumbukumbu namba ya malipo (control number);
b)Michango ya mwezi husika inapaswa kulipwa ndani ya mwezi husika au mwezi unaofuata;
c)Michango hiyo hulipwa na mwajiri na haitakiwi kukatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi;
d)Mapato ya mfanyakazi yanajumuisha mshahara (basic salary) na posho anazolipwa pamoja na mshahara na zisizobadilika;
e)Mwajiri ambaye hataleta mchango ndani ya muda ulioanishwa atalazimika kulipa riba ya asilimia mbili (2%) ya kiasi kilichocheleweshwa kwa mujibu wa kifungu cha 75 (2) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263], kikisomwa pamoja na kanuni ya 13 (7) ya Kanuni za Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi za mwaka 2016 na Kanuni ya 13 (7) ya Kanuni za Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Marekebisho ya mwaka 2021
f)Viwango vya uchangiaji vinavyopaswa kutumika katika kila kipindi cha mwaka wa fedha husika vitatangazwa kabla ya kuanza kutumika.