WCF TANZANIA YAANZISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA MIFUKO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI YA AFRIKA KUSINI

News Image

Imewekwa: 17th Jun, 2022

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Tanzania (WCF) umeanzisha ushirikiano wa kimkakati na Mifuko ya Fidia kwa Wafanyakazi AFRIKA Kusini ili kuboresha huduma za Fidia kwa wafanyakazi nchini.

Makubaliano hayo yamefanywa hivi karibuni jijini Dar es salaam kati ya WCF Tanzania na Mfuko wa Fidia wa Serikali wa Afrika Kusini pamoja na Mfuko wa Huduma za Fidia Rand Mutual Assurance.

Katika Mkutano huo, Mifuko yote mitatu imebainisha maeneo muhimu yakushirikiana ili kuendelea kuboresha huduma za Fidia kwa nchi zote. Pia wameainisha vipaumbele vitakavyotumika katika utelelezaji wa makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Huduma za Fidia Rand Mutual Assuarance kutoka Afrika Kusini, Bw. Mandra Shezi katika ofisi za WCF zilizopo jijini Dar es Salaam.

Tanzania Census 2022