Karibu

Mkurugenzi Mkuu - WCF

NENO LA UTANGULIZI

Karibu kwenye tovuti ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana, Wazee na wenye Ulemavu. Mfuko uliundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].

Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Tovuti yetu imeboreshwa ili kurahisisha upatikanaji wa moja kwa moja wa maudhui mbalimbali ikiwemo fomu, elimu juu ya Mfuko, sheria, mipangilio ya mada muhimu ambayo inahusu programu ya fidia kwa wafanyakazi nchini Tanzania pamoja na usajili wa mtandaoni.

Tunatarajia kuwa tovuti yetu iliyoboreshwa ni rahisi kwako kutumia na kutafuta maelezo yoyote muhimu unayohitaji kupata. Tunakaribisha maoni yako na tunaamini tovuti hii itakua ya manufaa kwako.

Masha J. Mshomba,

Mkurugenzi Mkuu