Malipo Ya Ulemavu Wa Kudumu

Mfanyakazi atapata fao la ulemavu wa kudumu endapo ataumia au kuugua kutokana na kazi na kumfanya apate ulemavu wa kudumu. Ulemavu wa kudumu humfanya mfanyakazi apoteze uwezo wa kufanya kazi na kusababisha asiweze kujipatia kipato tena katika maisha yake. Malipo haya yatatolewa kwa mfanyakazi mpaka atakapofariki au atakapofikia umri wa wa kustaafu na hivyo kuanza kupata malipo ya pensheni ya uzeeni endapo anastahili.