Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi

WCF Logo
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ndio. Mwajiri anaweza kupata taarifa ya michango yake kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa kuwasiliana na Mfuko.
Hapana. Mfuko unaendeshwa kwa mfumo wa bima yaani uchangiaji wa pamoja kwa lengo la kufidia watakaoathirika. Hivyo basi, michango iliyowasilishwa kwenye Mfuko hairudishwi kwa mwajiri.
Wanufaikaji wa Mafao yatolewayo na Mfuko ni: Wafanyakazi wote wanaoumia au wanaopata magonjwa kutokana na kazi ambao wapo katika Sekta Binafsi na Sekta ya Umma Tanzania Bara. Wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kwa ajali au ugonjwa unaotokana na kazi.
Mfuko ulianza kulipa fidia tarehe 01 Julai 2016.
Wafanyakazi wote walioumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kabla ya Tarehe 01 Julai 2016, madai yao yatashughulikiwa kwa utaratibu wa zamani kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ya Mwaka 1949 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya Mwaka...
Mafao yanayotolewa na Mfuko ni: Huduma ya matibabu Malipo ya ulemavu wa muda Malipo ya ulemavu wa kudumu Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa Huduma za utengemao Msaada wa mazishi Malipo kwa wategemezi
Huduma za matibabu zinazotolewa na Mfuko ni pamoja na: Huduma ya kusafirisha wagonjwa Kumuona daktari Uchunguzi Upasuaji Uuguzi Dawa Kurudia matibabu itakapobidi Viungo bandia
Taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo itatolewa kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz). Tukio la Ajali Mwajiriwa au mwakilishi wa Mwajiriwa anapaswa kutoa taarifa kwa Mwajiri ndani ya siku mbili (2) tokea tukio la ajali; Mwajiri baada ya kupokea taarifa hiyo au kutambua kutokea kwa ajali, ana...
Madai ya fidia yanapaswa kuwasilishwa katika Mfuko ndani ya kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) tokea tukio la ajali au kugundulika kwa ugonjwa.
Endapo Mwajiri atakataa kuwasilisha taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo katika Mfuko, Mfanyakazi au mwakilishi wa Wafanyakazi ana haki ya kuwasilisha taarifa hiyo katika Mfuko. Aidha, mwajiri kukataa kutoa taarifa ya tukio la ajali, ugonjwa au kifo ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wa...
Online Help
Adequate And Equitable Compensations
Chati Kupitia Whatapp
Wasiliana nasi kupitia Whatsapp
Unaitaji Msaada
Pata majibu ya hitaji lako hapa
Ndio. Mwajiri anaweza kupata taarifa ya michango yake kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa kuwasiliana na Mfuko.

" >
Hapana. Mfuko unaendeshwa kwa mfumo wa bima yaani uchangiaji wa pamoja kwa lengo la kufidia watakaoathirika. Hivyo basi, michango iliyowasilishwa kwenye Mfuko hairudishwi kwa mwajiri.

" >
Wanufaikaji wa Mafao yatolewayo na Mfuko ni:

  1. Wafanyakazi wote wanaoumia au wanaopata magonjwa kutokana na kazi ambao wapo katika Sekta Binafsi na Sekta ya Umma Tanzania Bara.
  2. Wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kwa ajali au ugonjwa unaotokana na kazi.
" >
Mfuko ulianza kulipa fidia tarehe 01 Julai 2016.

" >
Wafanyakazi wote walioumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kabla ya Tarehe 01 Julai 2016, madai yao yatashughulikiwa kwa utaratibu wa zamani kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ya Mwaka 1949 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya Mwaka 2002 kwa wafanyakazi wa sekta ya umma.

" >
Mafao yanayotolewa na Mfuko ni:

  1. Huduma ya matibabu
  2. Malipo ya ulemavu wa muda
  3. Malipo ya ulemavu wa kudumu
  4. Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa
  5. Huduma za utengemao
  6. Msaada wa mazishi
  7. Malipo kwa wategemezi
" >
Huduma za matibabu zinazotolewa na Mfuko ni pamoja na:

  1. Huduma ya kusafirisha wagonjwa
  2. Kumuona daktari
  3. Uchunguzi
  4. Upasuaji
  5. Uuguzi
  6. Dawa
  7. Kurudia matibabu itakapobidi
  8. Viungo bandia
" >
Taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo itatolewa kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz).

Tukio la Ajali

  1. Mwajiriwa au mwakilishi wa Mwajiriwa anapaswa kutoa taarifa kwa Mwajiri ndani ya siku mbili (2) tokea tukio la ajali;
  2. Mwajiri baada ya kupokea taarifa hiyo au kutambua kutokea kwa ajali, anapaswa kutoa taarifa kwenye Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) ndani ya siku saba (7) za kazi kuanzia siku ya tukio la ajali. Ili kuwezesha Mfuko kuthibitisha taarifa, mwajiri ataambatisha nakala ya mkataba wa ajira, taarifa ya namna tukio lilivyo tokea na taarifa ya polisi endapo ni ajali wakati wa safari (Conveyance) au inayohusisha tukio la jinai.

Tukio la Ugonjwa                                

  1. Mwajiriwa au mwakilishi wa Mwajiriwa anapaswa kutoa taarifa kwa Mwajiri ndani ya siku kumi na nne (14) za kazi tokea kutambulika kwa ugonjwa unaotokana na kazi;
  2. Mwajiri baada ya kupokea taarifa ya ugonjwa unaotokana na kazi, anapaswa kutoa taarifa kwenye Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) ndani ya siku saba (7) za kazi tokea siku ya kutambulika kwa ugonjwa. Ili kuwezesha Mfuko kuthibitisha taarifa mwajiri ataambatisha taarifa ya kitabibu ya uchunguzi wa ugonjwa na nakala ya mkataba wa ajira.

Tukio la Kifo

  1. Mwajiri au Mwakilishi wa Mwajiriwa aliyefariki, baada ya kupokea taarifa hiyo au kutambua kutokea kwa kifo, anapaswa kutoa taarifa kwenye Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa kujaza fomu (WCN 1) ndani ya kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) tokea siku ya ajali au kugundulika kwa ugonjwa;
  2. Ili kuwezesha Mfuko kuthibitisha taarifa, mwajiri ataambatisha taarifa ya tukio la ajali, nakala ya mkataba wa ajira, nakala ya cheti cha kifo, taarifa ya namna tukio lilivyo tokea, nakala ya kibali cha mazishi na taarifa ya polisi endapo ni ajali wakati wa safari (Conveyance) au inayohusisha tukio la jinai.
" >
Madai ya fidia yanapaswa kuwasilishwa katika Mfuko ndani ya kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) tokea tukio la ajali au kugundulika kwa ugonjwa.

" >
Endapo Mwajiri atakataa kuwasilisha taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo katika Mfuko, Mfanyakazi au mwakilishi wa Wafanyakazi ana haki ya kuwasilisha taarifa hiyo katika Mfuko. Aidha, mwajiri kukataa kutoa taarifa ya tukio la ajali, ugonjwa au kifo ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.

" >