Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi

WCF Logo
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ili kupata huduma, mfanyakazi atapaswa kuwasilisha Fomu (WCN -1) iliyojazwa kikamilifu na mwajiri pamoja na kitambulisho chake cha kazi afikapo hospitalini. Pamoja na fomu hiyo, kwa matibabu ya ugonjwa unaotokana na kazi Mfanyakazi ataambatisha barua iliyotolewa na Mfuko ili kumuwezesha kupata hudum...
Ulemavu ni hali ya kupungua au kupoteza uwezo wa kufanya kazi na hivyo kuathiri kipato cha mfanyakazi. Ulemavu upo wa aina mbili; Ulemavu wa muda hutokea katika kipindi ambacho Mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi anapokuwa amelazwa, kupatiwa siku za mapumziko ya kujiuguza...
Mfanyakazi, Mwajiri au Mwakilishi wa Mfanyakazi ana haki ya kuwasilisha maombi ya mapitio ya tuzo au uamuzi wa fidia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko ndani ya siku ishirini na moja (21) za kazi tangu alipopokea tuzo au uamuzi huo. Maombi hayo yawasilishwe kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa ku...
Mfanyakazi, Mwajiri, Mwakilishi wa Mfanyakazi au Mtu yeyote anaweza kuwasilisha maoni/maulizo/malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko kwa njia ya maandishi (barua pepe/ barua/tovuti), simu au kufika katika ofisi za Mfuko.
Mfuko Fidia kwa wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia maswala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tan...
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi upo katika Jengo la Victoria, Kitalu No. 37, Barabara ya Bagamoyo, Ghorofa ya 1 na 6 S. L. P 79655,Dar es Salaam. Muda wa Kazi: 2:00 asubuhi - 11:00 jioni  
Online Help
Adequate And Equitable Compensations
Chati Kupitia Whatapp
Wasiliana nasi kupitia Whatsapp
Unaitaji Msaada
Pata majibu ya hitaji lako hapa
Ili kupata huduma, mfanyakazi atapaswa kuwasilisha Fomu (WCN -1) iliyojazwa kikamilifu na mwajiri pamoja na kitambulisho chake cha kazi afikapo hospitalini. Pamoja na fomu hiyo, kwa matibabu ya ugonjwa unaotokana na kazi Mfanyakazi ataambatisha barua iliyotolewa na Mfuko ili kumuwezesha kupata huduma. Orodha ya watoa huduma na mahospitali husika inapatikana kwenye tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz)

" >
Ulemavu ni hali ya kupungua au kupoteza uwezo wa kufanya kazi na hivyo kuathiri kipato cha mfanyakazi. Ulemavu upo wa aina mbili;

  1. Ulemavu wa muda hutokea katika kipindi ambacho Mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi anapokuwa amelazwa, kupatiwa siku za mapumziko ya kujiuguza zaidi ya tatu (3) au kazi nyepesi kama itakavyoshauriwa na daktari;
  2. Ulemavu wa kudumu hutokea ambapo Mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi amepata ulemavu wa kudumu ambao umeathiri uwezo wake wa kutimiza majukumu yake ya kazi. Fidia hii hutolewa kwa mfanyakazi aliefikia ukomo wa matibabu
" >
Mfanyakazi, Mwajiri au Mwakilishi wa Mfanyakazi ana haki ya kuwasilisha maombi ya mapitio ya tuzo au uamuzi wa fidia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko ndani ya siku ishirini na moja (21) za kazi tangu alipopokea tuzo au uamuzi huo. Maombi hayo yawasilishwe kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa kujaza Fomu ya mapitio (WCC-5).

Aidha, endapo mleta maombi hataridhika na uamuzi wa mapitio wa Mkurugenzi Mkuu ana haki ya kuwasilisha maombi ya rufaa dhidi ya uamuzi huo kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi ndani ya siku

thelathini (30) za kazi tangu alipopokea uamuzi huo. Maombi hayo yawasilishwe kwa Fomu ya rufaa (WCC-6).

Vivyo hivyo, endapo mleta maombi atakuwa hajaridhika na uamuzi wa Waziri ana haki kuwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ndani ya siku sitini (60) za kazi tangu alipopokea uamuzi wa Muheshimiwa Waziri.

" >
Mfanyakazi, Mwajiri, Mwakilishi wa Mfanyakazi au Mtu yeyote anaweza kuwasilisha maoni/maulizo/malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko kwa njia ya maandishi (barua pepe/ barua/tovuti), simu au kufika katika ofisi za Mfuko.

" >