PROFESA NDALICHAKO ASHIRIKI KWENYE MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAZI NA AJIRA WA SADC MJINI LILONGWE

News Image

Imewekwa: 31st Mar, 2022

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Lilongwe nchini Malawi.

Katika mkutano huo uliofanyika Machi 30, 2022, Profesa Ndalichako alifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Maafisa wengine wa Serikali.

Aidha jumla ya ajenda 13 zilijadiliwa na Mawaziri hao ikiwa ni pamoja na kuweka Miongozo mbalimbali ya usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, Miongozo ya ukuzaji wa fursa za ajira na viwango vya kazi kwa nchi Wanachama na miongozo ya usimamizi mzuri wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.

Tanzania Census 2022