Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia maswala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania bara ambao wataumia,kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Madhumuni ya kuanzishwa kwa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi ni pamoja na:

  1. Kulipa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia ama kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo au kulipa fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi amefariki kutokana na ajali ama ugonjwa uliosababishwa na kazi aliyoajiriwa nayo.
  2. Kutekeleza matakwa ya Sera ya Hifadhi ya jamii ya mwaka 2003.
  3. Kutekele4za matakwa ya kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015.
  4. Kutoa huduma ya ukarabati na ushauri nasaha kwa wafanyakazi watakao umia ama kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo.
  5. Kuweka utaratibu utakaowezesha kuharakisha malipo ya fidia kwa wafanyakazi na wategemezi wao.
  6. Kuweka utaratibu mzuri wa kupokea michango kutoka kwa waajiri na kufanya malipo.
  7. Kukidhi matakwa ya Mikataba ya Kimataifa inayohusu fidia kwa wafanyakazi.
  8. Kukuza mbinu za kupambana na kuzuia ajali,magonjwa na vifo mahala pa kazi
hali ya kupungua au kupoteza uwezo wa kufanya kazi na hivyo kuathiri kipato cha mfanyakazi.
Ni malipo au huduma inayotolewa kwa mfanayakazi au wategemezi wa mfanyakazi baada ya mfanyakazi kupata ajali,ugonjwa ama kufariki kutokana na kazi aliyoajiriwa nayo.
Ni waajiri na wafanyakazi wote katika Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara.

Wajibu na Majukumu ya Mwajiri katika Mfuko ni kama yafuatayo:

  1. Kuifahamu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015
  2. Kujisajiri katika Mfuko
  3. Kulipa michango katika Mfuko kwa wakati.
  4. Kuimarisha usalama na afya mahala pa kazi
  5. Kutoa taarifa pindi mfanayakazi anapoumia,anapougua au kufariki kutokana na kazi
  6. Kutunza kumbukumbu na kuwasilisha taarifa za matukio ya ajali,magonjwa yanayotokana na kazi au vifokatika Mfuko kwa wakati
  7. Kuwafahamisha wafanyakazi kuhusu haki zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi
  8. Kuwasilisha katika Mfuko madai ya fidia kwa wafanyakazi kwa wakati pamoja na vielelezo vinavyohusu madai hayo.
  9. Kuweka sehemu wazi cheti cha usajili katika Mfuko ili wafanyakazi wajue kuwa mwajiri wao amejisajiri
  10. Kutoa taarifa katika mfuko kuhusu mabadiliko yoyote ya wafanyakazi ama vipato vyao.
  11. Kutoa ushirikiano kwa Mfuko ili uweze kufanya kazi zake kwa ufanisi kama vile kutoa ushirikiano wakati wa ukaguzi na kipindi cha kufanya tathmini ya mazingira hatarishi sehemu za kazi

Wajibu wa Mfanyakazi katika Mfuko ni:

  1. Kuifahamu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015]
  2. Kutoa taarifa kwa wakati kwa mwajiri au Mkurugenzi Mkuu pindi atakapopatwa na ajali kazini au kubainika kuwa na magonjwa yaliyotokana na kazi
  3. Kutoa ushirikiano pindi mfanyakazi anapotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu
  4. Kuzingatia maelekezo yatolewayo na Mamlaka mbalimbali kuhusu usalama mahali pa kazi
  5. Kuzingatia sheria,kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi
  6. Kutunza kumbukumbu binafsi zinazohusu masuala ya kazi
Kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi,mwajiri yeyote TAnzania Bara anatakiwa kujisajiri katika Mfuko
Mwajiri ana wajibu wa kuwafahamisha wafanyakazi wake haki zao pamoja na mafao watakayo pata kwenye Mfuko wa Fidia kwa kuweka tangazo na kutoa elimu akishirikiana na vyama vya wafanyakazi. Aidha, mfanyakazi ana haki ya kuwasiliana na Mfuko ili kupata uhakika endapo mwajiri wake amejisajiri katioka Mfuko
Mwajiri ana wajibu wa kuwafahamisha wafanyakazi wake kuhusu michango anayowachangia kwenye Mfuko.Aidha, mfanyakazi ana haki ya kuwasiliana na Mfuko moja kwa moja ili kujua kama mwajiri wake anawasilisha michango katika Mfuko