Kuanzishwa

UTANGULIZI
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].
Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.
MALENGO
Malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni pamoja na:
a)Kulipa fidia stahiki pale mfanyakazi atakapoumia, kuugua ama kufariki
b)Kutekeleza matakwa ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003
c)Kutekeleza matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015]
d)Kuweka utaratibu utakaowezesha kuharakisha malipo ya fidia kwa wanyakazi ama wategemezi wao
e)Kuweka utaratibu utakaowezesha Mfuko kupokea michango kutoka kwa waajiri na kufanya malipo
f)Kukuza na kuendelezambinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi
g)Kutoa huduma za ukarabati na ushauri nasaha
h)Kukidhi matakwa ya Mikataba ya Kimataifa kuhusu fidia kwa wafanyakazi.
MAJUKUMU
Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kama yafuatayo:
a)Kusajili waajiri
b)Kufanya tathmini ya mazingira hatarishi mahala pa kazi
c)Kukusanya na kupokea michango kutoka kwa waajiri
d)Kuwekeza michango itakayokusanywa
e)Kulipa fidia stahiki
f)Kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali, magonjwa na vifo mahala pa kazi
g)Kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi
h)Kutoa elimu kwa Umma kuhusu Mfuko