Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Mwajiri pekee ndiye anayechangia katika Mfuko.Mwajiri hapaswi kumkata mfanyakazi kiasi chochote cha pesa ,michango hii ni gharama ya mwajiri na sio mfanyakazi.
Viwango vya uchangiaji vinapatikana baada ya kufanyika kwa tathmini ya mazingira hatarishi sehemu za kazi
Kwa kipindi xcha mwaka wa fedha 2015/16 na mwaka wa fedha 2016/17,waajiri katika sekta Binafsi watachangia asilimia moja (1%) ya mapato ya wafanyakazi wao na waajiri katika Sekta ya Umma watachangia asilimia sifuri nukta tano (0.5) ya mapato ya wafanyakazi wao.Michango katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18 itawekwa wazi kabla ya tarehe 01 Julai,2017.
Mapato ya mfanyakazi yanajumuisha mshahara (basic salary) pamoja na posho anazolipwa na zisizo badilika mara kwa mara kutoka mwezi mmoja hadi mwingine.
ichango ya kila mwezi itawasilishwa ndani ya mwezi husika au mwezi unaofuatab (kwa mfano michango ya mwezi Julai itawasilishwa ndani ya mwezi Julai au Agosti lakini isizidi tarehe 30 Agosti) Aidha,Mwajiri anaweza akalipa kwa miezi mitatu ,sita au mwaka lakini baada ya kukubaliana na mkurugenzi Mkuu wa Mfuko.
Kama mdau mkuu katika Mfuko,Mwajiri anayo haki ya kupata taarifa ya michango aliyoiwasilisha kwenye mfuko.
Mfuko unaendeshwa kwa mfumo wa bima ,hivyo basi michango iliyowasilishwa kwenye Mfuko hairudishwi kwa mwajiri.