Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ndio. Mwajiri anaweza kupata taarifa ya michango yake kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwa kuwasiliana na Mfuko.
Hapana. Mfuko unaendeshwa kwa mfumo wa bima yaani uchangiaji wa pamoja kwa lengo la kufidia watakaoathirika. Hivyo basi, michango iliyowasilishwa kwenye Mfuko hairudishwi kwa mwajiri.
Wanufaikaji wa Mafao yatolewayo na Mfuko ni:
Wafanyakazi wote wanaoumia au wanaopata magonjwa kutokana na kazi ambao wapo katika Sekta Binafsi na Sekta ya Umma Tanzania Bara.
Wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kwa ajali au ugonjwa unaotokana na kazi.
Mfuko ulianza kulipa fidia tarehe 01 Julai 2016.
Wafanyakazi wote walioumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kabla ya Tarehe 01 Julai 2016, madai yao yatashughulikiwa kwa utaratibu wa zamani kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ya Mwaka 1949 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya Mwaka...
Mafao yanayotolewa na Mfuko ni:
Huduma ya matibabu
Malipo ya ulemavu wa muda
Malipo ya ulemavu wa kudumu
Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa
Huduma za utengemao
Msaada wa mazishi
Malipo kwa wategemezi
Huduma za matibabu zinazotolewa na Mfuko ni pamoja na:
Huduma ya kusafirisha wagonjwa
Kumuona daktari
Uchunguzi
Upasuaji
Uuguzi
Dawa
Kurudia matibabu itakapobidi
Viungo bandia
Taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo itatolewa kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz).
Tukio la Ajali
Mwajiriwa au mwakilishi wa Mwajiriwa anapaswa kutoa taarifa kwa Mwajiri ndani ya siku mbili (2) tokea tukio la ajali;
Mwajiri baada ya kupokea taarifa hiyo au kutambua kutokea kwa ajali, ana...
Madai ya fidia yanapaswa kuwasilishwa katika Mfuko ndani ya kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) tokea tukio la ajali au kugundulika kwa ugonjwa.
Endapo Mwajiri atakataa kuwasilisha taarifa ya ajali, ugonjwa au kifo katika Mfuko, Mfanyakazi au mwakilishi wa Wafanyakazi ana haki ya kuwasilisha taarifa hiyo katika Mfuko. Aidha, mwajiri kukataa kutoa taarifa ya tukio la ajali, ugonjwa au kifo ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wa...