IGP. CAMILLUS WAMBURA, AMEWATAKA WATENDAJI WA WCF KUWAJENGEA UELEWA MAKAMANDA WA POLISI

News Image

Imewekwa: 31st Jan, 2023

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amewataka watendaji wa WCF kuwajengea uelewa makamanda wa Polisi wa mikoa ili waweze kuelewa majukumu yao ni nini pale wanapohitaji taarifa kwa ajili ya kutoa fidia kwa wafanyakazi wanapoumia wakiwa katika kutekeleza majukumu yao.
IGP Wambura amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kinachohusisha makamanda wa Polisi wa mikoa kinachofanyika Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo makamanda hao wametakiwa kudumisha uhusiano na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na WCF.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, amesema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi umeanzishwa kwa mujibu wa sheria na lengo kuu la mfuko huo ni kulipa fidia kwa mfanyakazi au kumsaidia baada ya mfanyakazi kuumia au kufariki dunia kutokana na kazi.
Aidha, Dkt. Mduma amesema mfuko umewekeza katika kujenga ushirikiano na uhusiano wa kimkakati na taasisi mbalimbali zilizopo ndani na nje ya nchi sambamba na kuimarisha ushirikiano ambao umewezesha ubadilishanaji wa taarifa na uzoefu kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kiutendaji.