MADAKTARI WAASWA KUWA SEHEMU YA UTOAJI WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Paul Chacha ametoa wito kwa madaktari nchini kuwasaidia wafanyakazi wanaopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi zao kunufaika na huduma za fidia zinazotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mhe. Chacha ametoa rai hiyo hivi karibuni mjini Tabora wakati akifungua mafunzo kwa madaktari kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Tabora, Kigoma, Singida na Dodoma kuhusu tathmini za ulemavu unaosababishwa na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
“Mkumbuke, utendaji wenu bora utasaidia wafanyakazi wanaopata madhila yanayotokana na kazi zao kufanyiwa tathmini za ulemavu kwa wakati, kulipwa fidia stahiki na kwa wakati, na hivyo kuweza kurejea kazini mapema kuendeleza uzalishaji na kukuza tija kwa Taifa” alisema Mhe. Chacha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, alitoa wito kwa madaktari wanaoshiriki mafunzo hayo kuwahudumia wateja wa Mfuko huo kwa uadilifu na kuwasaidia kukamilisha taratibu zinazohitajika na WCF ili waweze kupatiwa stahiki zao kwa wakati.
“Wito wangu kwa madaktari ni kuendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi na kama watagundua ugonjwa wa mfanyakazi umetokana na kazi yake basi wamsaidie kukamilisha taratibu zinazohitajika WCF ili aweze kugharamiwa matibabu na kufanyiwa tathmini ya ulemavu kama upo ili aweze kulipwa fidia stahiki na kwa wakati,” alisema Dkt. Mduma.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisimbwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo aliwasisitiza madaktari kuwahudumia wagonjwa kwa weledi na kutoa taarifa za tathmini zinazotoa haki kwa pande zote, yaani wagonjwa, WCF na Serikali kwa ujumla.
“Ripoti zenu madaktari hasa za tahthmini ni muhimu sana kwani zitaisaidia WCF iweze kutoa haki kwa mhanga na pia kutosababisha hasara kwa Serikali,” alisema Dkt. Honoratha.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamefurahishwa na utaratibu wa WCF kutoa mafunzo hayo kwa kuwa yatawaongezea ujuzi na uelewa juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko huo na haswa fidia kwa wafanyakazi.
“Mafunzo haya yatatusaidia sisi madaktari kuwahudumia walengwa wa huduma zinazotolewa na WCF waliopo katika maeneo yetu ya kazi na hasa yale ya pembezoni,” alisema Dkt. Kassim Kolola; huku Dkt. Margreth Kwai akisema “katika maeneo tunayoyahudumia wapo wafanyakazi wanaopata ajali au magonjwa yanayotokana na kazi zao, lakini wengi hawakuwa na uelewa namna ya kusaidika, hivyo mafunzo hayo yametujengea uelewa wa masuala mbalimbali kuhusiana na WCF pamoja na namna ya kufanya tathmini ya ulemavu”.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umejiwekea utaratibu wa kutoa mafunzo hayo kote nchini ili kuhakikisha wanufaika wa huduma zake wanahudumiwa ipasavyo, ambapo hadi sasa takribani madaktari 2,000 wemekwisha kupata mafunzo ya awali (general medical practitioners training) na madaktari wasiopungua 130 wamepata mafunzo hayo kwa vitendo (hands-on impairment assessment training).