UZINDUZI NANENANE WANANCHI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI SENSA KWA MIPANGO BORA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

News Image

Imewekwa: 1st Aug, 2022

Serikali imefungua rasmi Maonesho ya Nanenane Kitaifa, Mbeya ikihimiza wananchi kushiriki katika Sensa ya Maendeleo na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2022.
Akizungumza Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema Nanenane 2022 ni sehemu sahihi ya kuelimisha wananchi kushiriki kwenye zoezi la Sensa 2022 ili kuwezesha Serikali kuwa na mipango bora kwenye Sekta ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ambayo ni miongoni mwa Sekta inayoshikilia sehemu kubwa ya uchumi wa wananchi walio wengi.
Katika ufunguzi huo amezipongeza Taasisi za Umma zilizo mstari wa mbele kuwezesha Maonesho hayo ambapo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni miongoni mwa washiriki wa Maonesho ya Nanenane 2022.
Naye Dkt. Abdulssalaa Omary mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF amesema katika Nanenane 2022, Mfuko huu utakutana na wadau wake na pia kutoa huduma kwa Waajiri na Wafanyakazi watakaotembelea Maonesho hayo.
Maonesho ya Nanenane kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya na yamefunguliwa rasmi tarehe 1 Agosti 2022.

Tanzania Census 2022