WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WAMILIKI WA VIWANDA KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI

News Image

Imewekwa: 26th Jul, 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefanya ziara mkoani Dar es laam kwenye maeneo ya kazi za Viwandani nakuwataka wamiliki wa viwanda kuzingatia matakwa ya Sheria za Kazi, ikiwemo Sheria ya Hifadhi ya Jamii, Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi pamoja na zinazohusiana na Mahusiano kazini.

Akiongea wakati wa ziara hiyo kwenye viwanda vitatu vinavyojishuhulisha na utengenezaji wa rangi na mabomba, Waziri Ndalichako amewapongeza wamiliki hao kwa kuendelea kutekeleza matakwa ya sheria na maelekezo ya Serikali na kuelekeza kushughulikia kasoro chache zilizobakia.

"Tayari kwenye baadhi ya viwanda nimegundua hakuna uwiano kati ya Wafanyakazi wanaolipiwa michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) naelekeza mrekebishe kasoro hizo," alisema Ndalichako

Mhe. Prof. Ndalichako amebainisha kuwa ni muhimu wamiliki wa Viwanda kuwalipia wafanyakazi wao WCF ili kuhakikisha wanalinda biashara zao dhidi ya majanga kwa wafanyakazi wao pindi wanapopata ajali au ugonjwa kutokana na kazi kwa ajili ya kupunguza migogoro isiyo ya lazima kazini na kuwezesha familia zao kujimudu wakati wa majanga.

Aidha, amebainisha kuwa katika baadhi ya viwanda amegundua wanawatumia Mawakala kuwalipa mishahara wafanyakazi wao, suala ambalo kwa Mawakala wanakuwa wanalitekeleza kinyume cha sheria na usajili wao, ambapo jukumu lao ni kumuunganisha Mfanyakazi na Taasisi. Utaratibu huo, huwapa changamoto waajiri kufuatilia juu ya makato.

Tanzania Census 2022