WAAJIRI JIUNGENI NA WCF KULINDA BIASHARA ZENU

News Image

Imewekwa: 19th Jun, 2022

Waajiri nchini wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kuwasilisha michango kwa wakati ili kulinda biashara zao dhidi ya majanga yanayoweza kuwapata wafanyakazi wao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.


Akizungumza baada ya Kikao Kazi na WCF, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO Bw. Gerson Msigwa amesema Mfuko huu ni moja kati ya Mifuko imara sana na yenye manufaa makubwa sana kwa waajiri na wafanyakazi.


"Niseme kwa ufupi, Afrika ni nchi chache sana zilizofanikiwa kuwa na Mfuko wa aina hii. Na imethibitishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuwa WCF Tanzania ni Mfuko himilivu wenye uwezo wa kulipa mafao kwa wafanyakazi kwa hadi mwaka 2048", amesisitiza Msemaji Mkuu wa Serikali.


Msemaji Mkuu wa Serikali pia ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kutoa huduma bora kwa wafanyakazi wanaopata ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi.


“Tunakupongeza Mkurugenzi Mkuu na timu nzima ya WCF, kwa kuandaa kikao kazi muhimu kwani imekuwa nafasi muafaka ya kufuatilia taarifa na mwenendo wa Mfuko huu katika utoaji huduma. Idara ya Habari - MAELEZO katika utendaji kazi wetu wa kuisemea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia imetusaidia kupanua wigo wa uelewa wa masuala ya fidia kwa wafanyakazi hususan takwimu” alisema Bw. Msigwa.

Ameongeza kuwa, Serikali imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha WCF inakuwa imara katika kutekeleza jukumu lake la kulipa fidia kwa wafanyakazi pasipo kuleta changamoto kwa waajiri. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015, WCF imeendelea kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wote wenye wanaopata madhira yanayotokana na kazi na viwango vya michango kutoka kwa waajiri pamoja na viwango vya fidia anayolipwa mfanyakazi vimeendelea kuboreshwa ili kukabiliana na changamoto halisi za maisha na uwekezaji.


“Tumeweza kupitia maboresho yaliyofanywa kwenye vipengele vya Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi sasa kazi iliyobakia kwetu ni kuelimisha jamii na watanzania juu ya nini wanatakiwa wafanye ili kustahili fidia kutoka WCF” alifafanua Bw. Msigwa.


‘Nitoe wito kwa waajiri wote nchini kulete michango kadiri inavyotakiwa. Tunajua wengi mnawasilisha lakini tuendelee ili tuweze kulinda biashara zetu kwa kuwalinda wafanyakazi wetu dhidi ya majanga kazini maana sio rahisi kujua ni wakati gani utapata madhara ama maradhi ukiwa kazini.


Mwajiri unapotoa michango ya wafanyakazi wako unachangia kumpa ujasiri mfanyakazi wako ambapo ataweza kufanya kazi bila hofu akijua inapotokea tatizo lolote basi WCF ipo kwa ajili yake na hiki ndio tungependa waajiri wote wakitekeleze.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema katika mwaka huu fedha, WCF inatarajia kutumia ..,. kulipa fidia kwa wafanyakazi waliopatwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi. Amefafanua kuwa kwa wafanyakazi waliofariki kutokana na kazi fidia hiyo iltalipwa kwa wenza wao pamoja na wategemezi wao ambapo watoto walio chini ya miaka 18 au wanaoendelea na masomo ngazi ya chuoni ni miongoni mwa wanufaika wa Mfuko huu.


Kuhusu mikakati ya utoaji wa elimu ya mafao ya fidia, Dkt. Mduma amesema Mfuko huu utaendelea kutoa elimu kupitia majukwaa tofauti ikiwemo Maonesho Sabasaba ambapo maafisa wake wakiwemo madaktari wabobezi wa tathimini za ulemavu ulitokana na kazi watakuwepo kwenye banda la Mfuko huo.

.Kikao kazi hicho kimekutanisha watendaji kutoka ofisi ya Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na watendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF.

Tanzania Census 2022