WCF YASHINDA TUZO MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI MWANZA

News Image

Imewekwa: 28th Aug, 2023

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umetwaa tuzo ya mshindi wa pili wa Mashirika, Wakala na Taasisi za Umma kwenye kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki jijini Mwanza (MEATF) 2023.

Maonesho hayo ambayo yamezinduliwa rasmi Agosti 28, 2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, yameandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), tawi la Mwanza yakilenga kuwaleta pamoja wadau wa masuala ya baishara katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zilizopo.

Sekta ya Viwanda na Biashara ni wadau wakubwa wa WCF kwani waajiri kutoka sekta ya Umma na Binafsi ni wanachama wa Mfuko huo ambao jukumu lake kubwa ni kulipa Fidia kwa mfanyakazi atakayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi alizoajiriwa kwa mujibu wa mkataba.