Michango

UCHANGIAJI
Waajiri wote katika Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara wanatakiwa kuchangia katika Mfuko. Mambo muhimu ya kuzingatia katika uchangiaji ni:
a)Kwa mujibu wa vifungu vya 74 (6) na 75 (1) vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015], kila mwajiri katika sekta binafsi na sekta ya umma Tanzania Bara anapaswa kuchangia katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
b)Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16, 2016/17 na 2017/18, michango ya waajiri imetengwa katika makundi mawili, yaani michango ya waajiri katika Sekta Binafsi na michango ya waajiri katika Sekta ya Umma
c)Michango katika Sekta Binafsi ni asilimia moja (1%) ya mapato ya wafanyakazi kwa kila mwezi
d)Michango katika Sekta ya Umma ni asilimia sifuri nukta tano (0.5%) ya mapato ya wafanyakazi kwa kila mwezi
e)Michango ya mwezi husika itawalishwa ndani ya mwezi husika au mwezi unaofuata na si vinginevyo.Ulipaji wa michango nje ya kipindi hiki ni ukiukaji wa matakwa ya kisheria
f)Waajiri wote kwa mujibu wa sheria wanatakiwa kuwasilisha michango kwenye Mfuko kwa niaba ya wafanyakazi wao. Aidha michango hiyo haitakiwi kukatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi
g)Mwajiri ambaye hataleta mchango ndani ya muda tajwa pamoja na kuwasilisha michango inayotakiwa, atapaswa kulipa riba ya asilimia kumi (10%) ya kiasi kilichocheleweshwa kwa mujibu wa kifungu cha 75 (2) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kikisomwa pamoja na kanuni ya 13 (7) ya Kanuni za Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi za mwaka 2016 na kanuni ya 7 (3) na (4) ya Tangazo la Serikali Na. 212A la tarehe 30 Juni 2016.
h)Pamoja na kulipa riba, mwajiri ambaye hatawasilisha michango ndani ya muda tajwa anaweza kulazimika atalazimika kulipa faini ya shilingi milioni 50 au kifungo cha miaka kumi (10) au vyote kwa pamoja. Adhabu hizi ni kwa mujibu wa vifungu vya 75 (3) na (4) vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015]
i)Viwango vya uchangiaji katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19 vitatangazwa kabla ya tarehe 1 Julai 2018
j)Fomu husika na maelezo kuhusu uwasilishwaji wa michango na malipo ya mafao vinapatikana katika Ofisi za Mfuko au katika Ofisi za Kazi zilizopo mikoa yote Tanzania Bara. Pia zinapatikana katika tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz). Aidha fomu za matibabu zinapatikana katika mahospitali, vituo vya afya na zahanati zenye makubaliano ya utoaji huduma za Mfuko.
k)Waajiri walio mikoani wanaweza kuwasilisha uthibitisho wa malipo pamoja na fomu zilizojazwa kwenye ofisi za Mfuko zilizopo Dar es Salaam, Kitalu Na. 37, “GEPF House”, Barabara ya Bagamoyo au kwenye ofisi za kazi zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.