Uanachama
USAJILI
Kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, mwajiri yoyote Tanzania Bara anawajibika kujisajili katika Mfuko.Mwajiri aliyekuwepo kabla ya tarehe 01 Julai 2015, aliwajibika kujisajili kwenye Mfuko tarehe 01 Julai 2015. Kwa Mwajiri aliyekuwepo baada tarehe 01 Julai 2015, anawajibika kujisajili kwenye mfuko ndani ya siku thelathini (30) baada ya kuajiri mfanyakazi wa kwanza.
Mwajiri anaweza kujisajili katika Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwakujaza Fomu za usajili (WCR-1 na WCR-2) na kuziwasilisha kwenye ofisi ya Mfuko iliyopo karibu nae au ofisi za idara ya kazi.