Slide background

TUPIGIE BURE SASA

TOLL FREE ~ HUDUMA KWA WATEJA:

0800110028 / 0800110029

kwa maswali yako yote kuhusu fidia kwa wanfanyakazi

Slide background

UMESHAWAHI KUKUMBWA NA HAYA KAZINI?

na mengine mengi ....

tutahakikisha unapata
huduma stahiki pamoja na fidia!

Slide background

MATIBABU

FIDIA KWA ULEMAVU

MSAADA WA MATIBABU ENDELEVU

FIDIA KWA WATEGEMEZI WALIOFIWA

Na Mengine Mengi ...

HABARI NA MATUKIO

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU MFUKO

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kuyafahamu kuhusu Mfuko Wa Fidia Kwa Wafanyakazi (yaani "Workers Compensation Fund" -WCF), ijapokuwa pia unaweza kuwasiliana nasi ama kututembelea kwa taarifa na ufafanuzi zaidi.

 1. Mfuko Wa Fidia

  Mfuko wa Fidia una jukumu la kufidia wafanyakazi ambao wamepata ajali za kikazi, magonjwa ama vifo vilivyosababishwa na utendaji wa kazi zao. Mfuko Wa Fidia unaendeshwa kwa taratibu za mifuko ya jamii, na ulianzishwa kwa sheria ya Fidia kwa wafanyakazi ya mwaka 2008 kifungu cha 20.

 2. Uanachama Na Vigezo

  Waajiriwa wote katika sekta za umma na sekta binafsi Tanzania bara wanahusika na hivyo waajiri wao wanapaswa kwa mujibu wa sheria kuchangia katika mfuko kwa niaba ya wafanyakazi wao. bofya hapa kujua zaidi kuhusu Uanachama

 3. Masharti

  Muombaji fidia lazima awe ni muajiriwa halali wa taasisi/kampuni anayotoka, lazima muajiri wake awe ni mchangiaji katika mfuko. Kwa vifo muombaji lazima awe mume/mke/tegemezi ambae mfanyakazi enzi za uhai wake alimuainisha kama tegemezi wake ama ndugu wa karibu. Baada ya ombi kutumwa, maafisa wetu watashughulikia ombi hilo kwa haraka iwezekanavyo, vilevile daktari pamoja na wataalamu wengine watashirikishwa kupitia dai hilo.

 4. Fidia Na Faida Zingine

  Muombaji ataweza kugharimiwa matibabu na kwa upande wa vifo wafiwa/tegemezi watapatiwa fidia kulingana na michango iliyokusanywa kutoka kwa muajiri. Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu fidia..

 5. Taratibu Za Kuomba Fidia

  Muombaji anapaswa kujaza fomu ikiambatanishwa na taarifa ya daktari/mtaalamu aliyeidhinishwa kupitia madai. Madaktari hawa walipatiwa mafunzo maalumu ya jinsi ya kupitia madai na kuwasilisha vielelezo kwa fidia kulipwa.

Wasiliana Nasi

 • Kitalu Na. 37, GEPF House, Ghorofa Ya 6

 • Br. Ya Bagamoyo., Regent Estate

 • S.L.P 79655

 • Dar es Salaam, Tanzania

 • Huduma Kwa Wateja:

 • +255 22 2926124/+255 22 2926125

 • Simu: +255 22 2926107/8

 • Fukushi: +255 22 2926109

 • BaruaPepe: info@wcf.or.tz