1. Madhumuni;
WCF ni Mfuko wenye dhamana ya kulipa fidia kwa wafanyakazi ama wategemezi wao endapo mfanyakazi ataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Aidha, Mifuko ya Pensheni, mathalani NSSF au PSSSF, ina dhamana ya kulipa mafao ya uzeeni pindi mfanyakazi anapostaafu kwa hiari au lazima.
Kwa upande mwingine, Mfuko wa Bima ya Afya mathalani NHIF una dhamana ya kutoa Bima ya matibabu kwa magonjwa yasiyotokana na kazi.
2. Uchangiaji;
Katika Mfuko wa WCF jukumu la uchangiaji ni la mwajiri pekee, wakati katika Mifuko mingine (PSSSF, NSSF & NHIF) jukumu la kuchangia lipo kwa Mwajiri na Mfanyakazi.
" >Aidha, OSHA ni mamlaka yenye dhamana ya kusimamia usalama na afya mahala pa kazi kwa kuhakikisha waajiri wote nchini wanaweka miundombinu na mifumo inayohakikisha usalama na afya mahala pa kazi vinalindwa.
" >Tukio la Ajali
Tukio la Ugonjwa
Tukio la Kifo
Aidha, endapo mleta maombi hataridhika na uamuzi wa mapitio wa Mkurugenzi Mkuu ana haki ya kuwasilisha maombi ya rufaa dhidi ya uamuzi huo kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi ndani ya siku
thelathini (30) za kazi tangu alipopokea uamuzi huo. Maombi hayo yawasilishwe kwa Fomu ya rufaa (WCC-6).
Vivyo hivyo, endapo mleta maombi atakuwa hajaridhika na uamuzi wa Waziri ana haki kuwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ndani ya siku sitini (60) za kazi tangu alipopokea uamuzi wa Muheshimiwa Waziri.
" >